• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China katika miezi 11 iliyopita wadumisha mwelekeo wa maendeleo ya utulivu

    (GMT+08:00) 2019-12-16 16:44:07

    Takwimu zinazotolewa na Idara ya Takwimu ya China zinaonyesha kuwa, katika miezi 11 iliyopita, uchumi wa China umeendelezwa kwa madhubuti na kudumisha mwelekeo wa maendeleo ya utulivu.

    Msemaji wa idara ya takwimu ya China Bw. Fu Linghui leo amesema, katika miezi 11 iliyopita, kiwango cha ongezeko la sekta ya viwanda kimeongezeka, maendeleo ya sekta ya viwanda vipya pia yanaharakishwa. Kuanzia mwezi Januari hadi Novemba, uwekezaji wa mali zisizohamishika kote nchini umefikia dola za kimarekani trilioni 7.62, ambayo ni ongezeko la asilimia 5.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Kuhusu hali ya sasa ya uchumi, Bw. Fu Linghui amesema,

    "Hayo yanaonyesha uchumi wa China una unyumbufu, nguvu na nafasi ya kubadilika chini ya hali tete ya kimataifa. Pia unapaswa kuona uchumi wa China uko katika kipindi kigumu cha kubadilisha mtindo wa maendeleo, kuboresha muundo wa uchumi na kubadilisha motisha ya ongezeko. Masuala ya mbalimbali kuhusu muundo, mfumo na mzunguko yanafungamana, uendeshaji wa uchumi unakabiliana na shinikizo la kupungua, katika kipindi kijacho, tunapaswa kufanya kazi sita za kutuliza uchumi, ili kuhimiza uchumi kuendelezwa vizuri."

    Aidha, kutokana na juhudi za pamoja za China na Marekani, makubaliano ya awali ya uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili yamefikiwa. Bw. Fu amesema, hii imepunguza wasiwasi katika soko, kuimarisha uaminifu wa soko, na pia itasaidia maendeleo ya uchumi wa China na dunia nzima.

    "Hivi sasa, makubaliano ya awali yamefikiwa, na kupunguza hali ya wasiwasi katika soko, ni vizuri kwa kuimarisha uaminifu wa soko na kuhimiza maendeleo ya uchumi na biashara, si kwa China tu, bali kwa Marekani, hata kwa dunia nzima. Juu ya hali ya jumla ya uchumi na biashara ya dunia kupungua, pande hizo mbili zimehimiza mazungumzo kwenye msingi wa kuheshimiana na kunufaishana, kuondoa hatua kwa hatua, ushuru unaoongezwa, na kutoa mchango zaidi kwa ajili ya ongezeko la uchumi duniani. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako