• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • New Zealand majogoo wa raga South Africa 7s

  (GMT+08:00) 2019-12-16 17:41:20

  New Zealand ndio mabingwa wapya wa duru ya Afrika Kusini ya Raga za Dunia za msimu 2019-2020 baada ya kuwafunga wenyeji Afrika Kusini 7-5 katika fainali kali zilizochezwa mjini Cape Town, Jumapili. Afrika Kusini, ambayo ilishinda duru hiyo kwa mara ya mwisho msimu 2015-2016, ilitangulia kufunga mguso bila mkwaju kupitia kwa Justin Geduld katika kipindi cha pili. Hata hivyo, Ngarohi McGarvey-Black alisawazisha na mguso ulioandamana na mkwaju kutoka kwa Akuila Rokolisoa. Timu ya Kenya almaarufu Shujaa ilimaliza ziara ya Cape Town katika nafasi ya saba kwa alama 11. Shujaa ya kocha Paul Feeney sasa ina jumla ya alama 15, ilikuwa imezoa alama nne pekee katika duru ya ufunguzi mjini Dubai wiki moja iliyopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako