• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Wang Qishan ataka kuzidisha maelewano kati ya watu wake na dunia

    (GMT+08:00) 2019-12-16 20:38:29

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan leo amekutana na waliokuwa viongozi wa nchi mbalimbali na mabalozi wa nchi za nje akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Japan Bw. Yukio Hatoyama ambayo wamehudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 70 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya mambo ya nje ya watu wa China mjini Beijing.

    Wang amesema inapaswa kuzidisha maelewano kati ya watu wa China na wa dunia, kuhimiza mawasiliano, mazungumzo na ushirikiano kati ya pande mbalimbali, na kutoa mchango zaidi kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa dunia. Ameongeza kuwa, serikali ya China daima inatilia maanani mambo ya diplomasia yasiyo ya kiserikali, na kwamba ni muhimu kuimarisha msingi wa urafiki kati ya watu wa nchi mbalimbali chini ya hali ya sasa ya kimataifa yenye mabadiliko.

    Naye Yukio Hatoyama amesema Japan itaendelea kutoa mchango wake katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili pamoja na urafiki kati ya watu wa nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako