• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Umeme yapokea mikopo ya kuboresha huduma zake

  (GMT+08:00) 2019-12-16 20:54:40
  Kampuni ya kusambaza umeme nchini Uganda Umeme imepata mkopo wa dola milioni 70m kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), Benki ya Maendeleo ya Uholanzi FM, benki ya Stanbic na Benki ya Standard Chartered.

  Mwenyekiti wa Umeme, Bwana Patrick Bitature amesema mkopo huo utatumika kuwekeza kenye usambazaji wa umeme kutoka mabwawa mapya nchini humo.

  Umeme pia inasema mkopo huo utatumika kuweka kipaumbele uwekezaji katika maeneo mengine matano ikiwa ni pamoja na kusambaza kawi viwandani, kuboresha mtandao wake, kujenga jukwaa la kuunganisha zaidi umeme na kupunguza upotezaji wa nishati.

  Kwa sasa upoteaji wa nishati ni asilimia 16.9 lakini upotezaji wa kibiashara ambao unaotokana na viunganisho haramu ni karibu asilimia 5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako