Mkurugenzi Mtendaji wa mji wa kisasa wa Konza John Tanui, amesema kituo hicho ni sehemu muhimu ya jiji hilo na pia kitakuwa kituo cha data cha kitaifa.
Alisema kituo hicho cha data kitakuwa muhimu kwa mchakato wa kitaifa wa dijitali na kitatoa jukwaa la kuhifadhi data inayohitajika ili kukuza uchumi.
Tanui amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kituo cha Luban katika chuo kikuu cha Machakos.
Kituo hicho ni hatua ya kwanza ya ujenzi wa jjumla ya mji wa Konza na kinatarajiwa kufungua nafasi 20,000 za ajira.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |