• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzalishaji wa viwandani China waongezeka

    (GMT+08:00) 2019-12-16 20:55:45

    Uzalishaji wa viwandani wa China, ambao ni ishara muhimu ya uchumi,uliongezeka kwa asilimia 5.6 katika miezi 11 ya kwanza ya mwaka 2019.

    Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa (NBS) imesema mazao ya viwandani yalipanda asilimia 6.2, kutoka asilimia 4.7 uliosajiliwa Oktoba.

    Pato la viwanda la China, linaloitwa rasmi thamani ya viwandani, hutumika kupima shughuli kubwa za biashara kubwa zenye angalau mapato ya Yuan milioni 20 kila mwaka (karibu milioni 2.86 dola za Kimarekani).

    Msemaji wa kituo hicho cha taakwimu Fu Linghui amesema ukuaji wa pato la Novemba ulionyesha maendeleo thabiti ya viwandani na uboreshaji.

    Kampuni binafsi ziliongezeka kwa asilimia 8.9 kimapatohasa zikinufaika na hatua ya serikali inayounga mkono wafanyabiashara wadogo na wa kati.

    Nao uzalishaji na usambazaji wa umeme, kawi ya mvuke, gesi na maji ziliongezeka kwa asilimia 6.7 mnamo Novemba, ambayo ni ya kwanza kati ya sekta tatu kuu, ambazo ni pamoja na madini na utengenezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako