• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Mashamba ya NYS nchini Kenya yatatumika kwa upanzi wa mbegu

  (GMT+08:00) 2019-12-16 20:56:42
  Mashamba yote ya Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) nchini Kenya yatatumika kwa upanzi wa mbegu za mimea mbalimbali.

  Hii ni baada ya kutekelezwa kwa mradi wa majaribio wa upanzi wa viazi kwenye shamba la shirika hilo katika Kaunti ya Nyandarua.

  Mamia ya wakulima walifika shambani humo kujionea mbegu za viazi zilizokuzwa na kujifunza mengi kuhusu kilimo.

  Akizungumza shambani humo, Mkurugenzi mkuu wa NYS Matilda Sakwa alisema shirika lake linaendelea kushauriana na Idara ya Kilimo ya Ukuzaji wa Mbegu na Ustawishaji wa Mimea (Kephis) ambayo ilichangia ufanisi wa mradi huo wa majaribio.

  Aidha NYS itawauzia wakulima mbegu hizo kwa bei ya chini ikilinganishwa na kiwango kilichowekwa na kampuni nyingine za kuuza mbegu nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako