• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Serikali yapanga kuongeza idadi ya watalii

  (GMT+08:00) 2019-12-16 20:57:05
  Naibu waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Constantine Kanyashu amesema Serikali kwa inaendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza idadi ya watalii kutoka milioni 1.6 hadi milioni 2.4 ifikapo mwaka 2022.

  Akizungumza katika mahafali ya 17 ya Chuo cha Taifa cha Utalii jijini Dar es Salaam, Kanyashu ameitaja mikakati hiyo ni pamoja na kuongeza hifadhi za Taifa, ununuzi wa ndege na kuboresha miundombinu ya vivutio vya utalii.

  Amesema serikali pia imeboresha miundombinu kwa kujenga barabara na imenunua ndege za kutosha.

  Akieleza umuhimu wa sekta hiyo, Kanyashu amesema mpaka sasa inachangia pato la fedha za kigeni kwa asilimia 25 na asilimia 17.5 ya pato la ndani (GDP).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako