• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afya ya Apolot yaimarika baada ya matatizo ya moyo

  (GMT+08:00) 2019-12-17 16:52:01

  Mshindi wa mchezo wa kick boxing kwa wanawake nchini Uganda Patricia Apolot ameonekana kuwa na afya njema baada ya kulalamikia maumivu makali ya kifua ambayo yalihusishwa na mshtuko mdogo wa moyo wakati akiwa kwenye mazoezi kwenye kambi iliyoko Ngora, Teso, wiki iliyopita. Hali hiyo ilisitisha mazoezi yake kwa kuwa alitakiwa kusafiri hadi Kampala kwa ajili ya matibabu ya maumivu makali ya kifua, ambayo ni ishara kubwa ya mshtuko wa moyo. Apolot amesema, anaendelea na matibabu, na kwamba tiba aliyoitumia haimzuii kufanya mazoezi. Kwa sasa, Apolot ndio amechukua tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kike wa Kick Boxing iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako