• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ripoti yaonyesha kampuni zinataka kuboresha zaidi sera za kupunguza gharama

  (GMT+08:00) 2019-12-17 19:42:57

  Ripoti ya kutathmini mizigo ya kampuni za China ya mwaka 2019 imeonyesha kuwa, hatua mbalimbali zilizotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali la China kuhusu kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kupunguza mizigo ya kampuni zimepata matokeo mazuri, na mazingira ya maendeleo ya kampuni yameboreshwa zaidi. Lakini kutokana na kuongezeka kwa shinikizo la kushuka kwa uchumi, kampuni hizo zinataka kupunguza zaidi gharama.

  Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, katika kampuni zilizojibu dodoso, asilimia 45 zinaona zina mizigo mingi, idadi ambayo imepungua kwa asilimia 12 kuliko mwaka jana, asilimia 26 ya kampuni zinaona mizigo yao imepungua kuliko mwaka uliopita, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 12.

  Naibu mkurugenzi wa kituo cha kuhimiza maendeleo ya kampuni za ndogo na za ukubwa wa kati nchini China Bw. Luo Junzhang amesema, uchunguzi huo umeweka vigezo husika kulinganishwa na ripoti ya mazingira ya kufanya biashara ya Benki ya Dunia, zikiwemo ushuru, ada, biashara za kiutaratibu, mambo ya fedha na vigezo vingine 23 katika pande 8. Anasema,

  "Matokeo yanaonyesha kuwa, mambo yanayoridhisha na yanayoridhisha sana kwa kampuni ni pamoja na urahisi wa kuanzisha kampuni na kubadili habari za usajili wa kampuni, urahisi wa kupata umeme na ulinzi wa hakimiliki za ujuzi, ambazo zimechukua asilimia 90, asilimia 97 na asilimia 87. Na urahisi wa kupata mikopo hauridhishi. "

  Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, chini ya kuongezeka kwa shinikizo la kushuka kwa uchumi, kampuni zina mahitaji zaidi ya kupunguza gharama, zinataka serikali kuendelea kutoa sera za kupunguza ushuru, kupunguza gharama za uwekezaji na kupanua njia ya kupata wawekezaji, kupunguza gharama za kutumia nishati na ardhi na gharama za uchukuzi, kufuta mchakato wa idhini usio lazima na kupunguza gharama za biashara ya kiutaratibu.

  Aidha, ripoti hiyo pia inapendekeza kuimarisha ujenzi wa mfumo wa huduma za umma, ujenzi wa usimamizi wa masuala yanayohusiana na vitendo haramu, kujenga mfumo wenye ufanisi wa muda mrefu wa kukinga na kutatua suala la kushindwa kupatikana kwa fedha.

  Kampuni 6,188 kutoka mikoa 31 kote nchini zimejaza dodoso , na asilimia 70 ni za kampuni binafsi, kampuni zenye ukubwa wa kati na ndogo zimechukua asilimia 88.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako