• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha televisheni cha Italia chafanya mahojiano na mkuu wa Shirika kuu la Utangazaji la China (CMG)

    (GMT+08:00) 2019-12-17 20:25:53

    Kituo cha televisheni cha Italia TGCOM24 limefanya mahojiano na mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong, ambaye alizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo mageuzi ya vyombo vya habari, uchumi wa China, biashara kati ya China na Marekani na suala la Hong Kong.

    Bw. Shen amesema kwa sasa CMG inabadilika kuwa shirika la vyombo vya habari vipya lenye kiwango cha juu zaidi duniani linayotengeneza na kutangaza vipindi vya sauti na video. Kuhusu suala la uchumi wa China, amesema ongezeko la pato la taifa la China linakadiriwa kufikia asilimia 6.1 mwaka huu, ambayo itafikia takriban dola elfu kumi za kimarekani kwa mtu.

    Akizungumzia suala la biashara kati ya China na Marekani, Bw. Shen amesema kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu kunatakiwa ushirikiano wa kunufaishana. Anaamini kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea vizuri.

    Kuhusu Hong Kong, Shen amesema baadhi ya wanasiasa na wadau wa Marekani wanataka kuzuia maendeleo ya China na maendeleo ya China bara kwa kutumia suala la Hong Kong. Ameongeza kuwa, serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong na watu wa Hong Kong wanaweza kutatua suala la Hong Kong kwa uungaji mkono wa serikali kuu ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako