Wachumi wanasema mabadiliko ya sera hiyo yanaambatana na hali ya sasa ya ulimwengu ambapo benki kuu zinapunguza viwango vya riba kupiga jeki ukuaji katika hali duni ya uchumi wa Dunia.
Benki ya Dunia inatarajia ukuaji wa wastani wa pato la Taifa katika nchi za Afrika kupungua hadi asilimia 5.9 mwaka huu kutoka asilimia sita mwaka jana, kwa sababu ya hali ya misukosuko katika masoko ya kimataifa na Kenya, Uganda, na Rwanda kurekodi viwango vya ukuaji wa wastani ikilinganishwa na mwaka jana.
Uchumi wa Tanzania na Burundi unatarajiwa kukua haraka mwaka huu kuliko mwaka wa 2018, kulingana na taasisi ya Bretton-Woods.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |