• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa taifa wa China Bw. Wang Yong akutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

  (GMT+08:00) 2019-12-18 09:01:16

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumatatu alikutana na mjumbe maalumu wa rais wa China Bw. Wang Yong ambaye yuko nchini Kenya kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa mradi wa awamu ya kwanza wa reli kati ya Nairobi na Malaba.

  Bw. Wang Yong amewasilisha salamu za rais Xi Jinping kwa rais Kenyatta, na kusema katika miaka ya hivi karibuni marais hao wawili wamekutana mara nyingi na kufikia makubaliano mengi kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye nyanja mbalimbali, na kuuelekeza uhusiano kati ya China na Kenya kwenye zama mpya. Pia ameeleza imani yake kuwa chini ya uongozi na ufuatiliaji wa viongozi wa nchi hizo mbili, uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Kenya utaendelea kupiga hatua na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili na watu wa Afrika kwa ujumla.

  Kwa upande wake rais Kenyatta amesema Kenya inathamini urafiki kati yake na China, na inapenda kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yake na China, kupanua ushirikiano kati ya nchi mbili kwenye sekta ya biashara, uwekezaji na miundombinu, kuongeza uratibu kwenye mambo ya kikanda na ya kimataifa, ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja na kutimiza lengo la kunufaishana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako