• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Dau la Zaha laziweka mtegoni Chelsea, Everton

  (GMT+08:00) 2019-12-18 16:15:02

  Klabu za Chelsea, Arsenal na Everton zitalazimika kutoa paund milioni 80 kupata saini ya nyota wa Crystal Palace, Wilfred Zaha. Mchezaji huyo amekuwa akisisitiza kuwa anataka kuondoka Palace katika usajili wa dirisha dogo mwezi ujao baada ya kucheza kwa kiwango bora kwa karibu misimu miwili. Hata hivyo, Palace imetoa masharti kwa klabu inayomtaka kuwa mchezaji huyo atauzwa kwa paundi milioni 80, vinginevyo ataendelea kubaki kwenye klabu hiyo. Timu za Chelsea, Arsenal na Everton zimekuwa zikiwinda saini ya mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ivory Coast bila mafanikio. Wakati hayo yakiendelea, klabu ya Manchester United yenyewe imekubali kutoa pound milioni 76 kumsajili mshambuliaji kinda wa Redu Bull Salzburg, Erling Haaland mwezi ujao katika dirisha dogo la usajili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako