• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti yaonyesha nchi nyingi zikipokea mapato kidogo ya ushuru

    (GMT+08:00) 2019-12-19 18:03:58

    Ripoti ya utafiti uliofanywa kuhusu soko huria barani Afrika inasema kuwa nchi nyingi za Afrika hazitakuwa na mapato mengi katika soko hilo. Ripoti hiyo ambayo iliwasilishwa na mawaziri wa biashara barani Afrika nchini Ghana inasema mapato ya kodi yatashuka hadi chini ya asilimia 1.5 isipokuwa nchi za Jamhuri ya Kongo, Gambia na Zambia.

    Wakati huo huo, suala la upatikanaji masoko kwa bidhaa zinazozalishwa Afrika ni miongoni mwa changamoto zinazozikabili nchi zilizopo barani Afrika hivyo kuzifanya zitegemee zaidi masoko ya nje.

    Masoko ya nje kwa bidhaa na huduma zinazotoka Afrika zimekabiliwa na vikwazo vikiwamo viwango vikubwa vya ubora visivyolingana na teknolojia za uzalishaji kwenye nchi hizo. Mazingira ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na upatikanaji duni na usiokuwa wa uhakika wa nishati, ubovu wa miundombinu kama barabara, teknolojia duni na mengineyo kama hayo, yamesababisha bidhaa na huduma zinazozalishwa barani Afrika kushindwa kuhimili ushindani kwenye soko la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako