• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Banki kuu ya Tanzania yapongeza benki ya ICB

  (GMT+08:00) 2019-12-19 18:04:23

  Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse, ameipongeza Benki ya Biashara ya Kimataifa (ICB) kwa jitihada zake za utoaji wa mikopo kwa wateja wake hali ambayo inachochea ukuaji wa uchumi nchini.

  Akizungumza katifa hafla ya kuadhimisha miaka 22 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo, Dk.

  Kibesse, alisema benki hiyo imetekeleza vizuri wajibu wake kwa kutoa mikopo na ushauri kwa wateja wake.

  Alisema BoT itaendelea kushauri benki ziweze kufika maeneo mbalimbali ya nchi hususan vijijini ili kuongeza watumiaji wa huduma za kibenki hapa nchini.

  Dk. Kibesse alieleza kwa sasa hali ya utoaji mikopo kwa benki imeimarika ukilinganisha na miaka miwili iliyopita na hivyo kuonyesha taswira nzuri ya kuimarika kwa uchumi.

  Mmoja wa wabia wakuu wa Benki ya ICB Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi, Josephine Sevaretnam, alisema wameridhishwa na mazingira ya kiuwekezaji yaliyopo Tanzania na wamejipanga kuboresha zaidi huduma zao.

  Aidha, alieleza matumaini yake kwa serikali ya Tanzania na sekta ya kibenki kwa namna inavyoweka mipango yake kwa kushirikisha wadau jambo ambalo limewapa nguvu zaidi ya kuwekeza Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako