• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mabasi ya Modern Coast yanayohudumu Afrika mashariki yanaswa nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2019-12-19 18:04:41
  Abiria 90 waliokuwa wakisafiri kwa mabasi mawili ya kampuni ya Modern Coast walilazimika kukwama katika barabara kuu ya Mombasa baada ya polisi kunasa mabasi hayo.

  Mabasi hayo yalikuwa yakisafiri kutoka Mombasa kuja maeneo ya bara licha ya marufuku iliyowekwa dhidi yao na Mamlaka ya Usalama Barabarani (NTSA) wiki jana.

  Kampuni hiyo inadaiwa kupokonywa leseni ya kuhudumu baada ya mabasi yake mawili kugongana eneo la Kiogwani katika barabara kuu Mombasa- Nairobi ambapo watu saba walifariki. Watu wengine 60 walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa sita za usiku Jumatano wiki jana.

  Aidha Jumanne kulitokea habari za kukanganya kwamba NTSA imeondoa marufuku dhidi ya kampuni hiyo ya Modern Coast na kuhusu mabasi yake kurejelea huduma. Hata hivyo mamlaka hiyo ilikana madai hayo.

  Awali kampuni hiyo ilikuwa imesema kwamba NTSA imeirejeshea leseni ya kuhudumu baada ya kukagua mabasi yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako