Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amesema Baraza la Mawaziri lilitengeneza ratiba ya jinsi pesa inayodaiwa na wizara, idara za serikali na mamlaka italipwa.
Dk Matiang'i ameanika magavana wa kaunti 15 kwa kushindwa kulipa deni zao licha ya kupokea pesa kutoka Hazina.
Ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa niaba ya Hazina ya Kitaifa mwaka jana ilionyesha kuwa serikali za kitaifa na za kaunti zinadaiwa na wauzaji zaidi ya Sh bilioni 225 zilizo nyuma miaka kadhaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |