• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Meli ya hospitali ya China yatoa matibabu kwa watu wa nchi za nje

  (GMT+08:00) 2019-12-23 18:13:57

  Meli ya "Safina ya Amani" ni meli ya kwanza ya hospitali ya jeshi la majini la China. Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita tangu ijiunge na jeshi la China, meli hiyo imetembelea nchi 43 na kutoa huduma za matibabu kwa watu laki 2.3 wa nchi hizo.

  Hadi sasa meli ya hospitali ya "Safina ya Amani" imetoka nje ya China mara tisa, na kusafiri zaidi ya kilomita laki 4.3. Kamishna wa meli hiyo Chen Yangyang ameeleza kuwa, licha ya kutoa huduma kwa jeshi la China, meli hiyo ina majukumu mengine maalumu, anasema,

  "Jukumu letu la kwanza ni kutoa huduma za kibinadamu za matibabu duniani. La pili ni uokoaji katika maafa makubwa, kwa mfano kimbunga Haiyan kilichoikumba Philippines mwaka 2013. Na la tatu ni kufanya ushirikiano wa kimataifa wa matibabu. Katika miaka zaidi ya 10 iliyopita, tumekwenda sehemu yoyote tuliyohitajika, ikiwemo nchi zenye ugonjwa wa Ebola barani Afrika, na Philippines iliyokumbwa na kimbunga kikubwa."

  Kuanzia tarehe 31, Agosti hadi tarehe 26 Novemba mwaka 2010, meli hiyo ilifanya ziara yake ya kwanza katika nchi tano zikiwemo Djibouti, Kenya, Tanzania, Shelisheli na Bengal. Katika bandari ya Jeddah nchini Bengal, hospitali ya kienyeji iliomba msaada kwa meli hiyo, kwani kulikuwa na mama mja mzito mwenye ugonjwa wa moyo na alikuwa anahisi kujifungua kabla ya wakati wake, hivyo alihitaji kufanyiwa upasuaji. Madaktari wa China walikwenda hospitali hiyo mara moja, na kumsaidia mwanamke huyu kujifungua salama. Mtoto huyu akapewa jina la "China".

  Mwezi Novemba mwaka 2013, katika sehemu ya Paro iliyoathiriwa zaidi na kimbunga Haiyan nchini Philippines, madaktari wa meli hiyo hawakurudishwa nyuma na mazingira magumu ikiwemo magonjwa ya kuambukiza, maji machafu, mbu na nzi. Walifanya kazi saa 24 kila siku kwa siku 16 mfululizo, na kuwatibu watu 2,208 waliojeruhiwa. Licha ya kutoa matibabu bure, pia waliwasaidia waathirika kukagua maji, na kuwapa dawa ya kukinga maradhi. Katika miaka zaidi ya 10 iliyopita, meli hiyo pia imewasaidia zaidi ya watu 500 wenye ugonjwa wa mtoto wa jicho kuona tena. Daktari wa meli hiyo Wu Jinhui anasema,

  "Tulimfanyia bibi mmoja wa Afrika upasuaji wa ugonjwa wa mtoto wa jicho. Siku ya pili alinikumbatia na kunishukuru sana. Hakusema maneno mengi, lakini alinikumbatia kwa muda mrefu. Nilifurahi sana"

  Kamishna wa meli hiyo Chen Yangyang anasema,

  "Tumefanya kazi za kibinadamu, na tumeeneza mawazo ya kidiplomasia ya nchi yetu, yaani amani, maendeleo, ushirikiano na mafanikio ya pamoja. Aidha tumeonesha urafiki, uzuri na amani ya watu wa China kwa watu wa dunia, ili waweze kufahamu vizuri zaidi China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako