• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Simu gushi kufungwa Uganda

    (GMT+08:00) 2019-12-23 19:16:44

    Serikali ya Uganda imeanza mchakato wa kuzima simu bandia baada ya kuanza kutumia mitambo mipya ya kutambua bidhaa za elektroniki ambazo hazijatimia viwango.

    Hatua ya Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) inafuatia kuongezeka simu bandia katika soko la Uganda katika miezi michache iliyopita.

    Mkurugenzi wa mawasiliano wa UCC Ibrahim Bbosa, amesema mitambo hiyo mipya itaungwanishwa moja kwa moja na kampuni za uuzaji na huduma za simu.

    UCC imesema mfumo huo utaunganisha watumiaji wa simu chini ya orodha tatu tofauti- orodha nyeupe ambayo itakuwa na simu za zinazotimia viwango, orodha ya kijivu ambayo itakuwa na simu ambazo zinaweza kutumika kwa zaidi ya nchi moja na na orodha nyeusi ambayo ni simu gushi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako