• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Uuzaji nje wa parachichi waongezeka hadi asilimia 39

  (GMT+08:00) 2019-12-23 19:17:07

  Wakulima wadogo wadogo nchini Kenya wanaweza kuongeza mapato yao kwa karibu asilimia 39 kwa kuuza parachichi katika soko la Ulaya.

  Kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Chakula ya Kimataifa parachichi aina ya Haas ambazo huuzwa kwenye soko la ndani kwa shilingi tatu, zinaweza kuuzwa kwa shilingi 6 kwenye masoko ta nje.

  Hata hivyo wakulima wa wadogo wa parachichi hawawezi kuchukua fursa ya bei kubwa kutokata na ukosefu wa mtaji wa kutosha, miundombinu duni na gharama kubwa ya kukidhi viwango vikali vya usafirishaji.

  Kulingana na taasisi hiyo ni wakulima wachache wa parachichi, wengi katika kaunti ya Muranga katikati mwa Kenya, wanaounganishwa na masoko ya kuuza nje kupitia kilimo cha mikataba.

  Licha ya kuongezeka kwa mahitaji ya kimataifa, usafirishaji wa matunda hayo kutoka Kenya umekuwa ukipungua.

  Biashara ya parachichi imekuwa na faida nchini Kenya kufuatia mahitaji ya matunda hayo ulimwenguni kote kutokana na uelewa mkubwa wa faida zake za kiafya.

  Kenya ni mzalishaji wa pili mkubwa wa avocados barani Afrika, baada ya Afrika Kusini.

  Inauza mazao hayo kwa Falme za Kiarabu, Uingereza, Misri, Uholanzi, Ufaransa, Saudi Arabia, Ubelgiji, Uhispania, Qatar, Bahrain, Kuwait, Ujerumani na China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako