• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: KRA yakusanya shilingi bilioni 629 kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2019/2020

  (GMT+08:00) 2019-12-23 19:17:26

  Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) imekusanya zaidi ya Shilingi bilioni 628 kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2019/2020.

  Ushuru huo unawakilisha asilimia 36 ya matarajio ya shilingi trilioni 1.7 yaliyowekwa kwa mwaka 2019/20.

  Kulingana na taarifa ya hivi karibuni zamapato na matumizi yaliyotolewa na wizara ya fedha, jumla ya Shilingi trilioni 1 kutoka mpango wa matumizi ya Shilingi trilioni 2.6 kwa mwaka huu wa fedha tayari zimetolewa.

  Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 389 bilioni zimetolewa kwa wizara na idara mbali mbali za serikali - ambazo zinawakilisha asilimia 40 ya mgao wa Shilingi trilioni 1 kwa mwaka huu wa fedha.

  Mwaka jana, KRA ilikosa malengo ya ukusanyaji wa mapato na kwa shilingi bilioni 100, na hivyo kuilazimu wizara ya fedha kupendekeza hatua za ziada za ushuru katika Muswada wa Fedha wa 2019/2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako