• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Somalia: Waziri wa utalii somalia apongeza ukuaji wa uchumi

  (GMT+08:00) 2019-12-23 19:17:49

  Serikali ya Somali imesema imefikia malengo muhimu kwa uchumi, usalama na kisiasa ambayo yameweka msingi wa kutosha wa kusukuma nchi mbele mwaka2020.

  Waziri wa habari, utamaduni na utalii Mohamed Abdi Hayir, amesema uchumi ulikua kwa asilimia 3.8 mwaka 2019 na anatarajia ukuaji zaidi mwaka ujao kutokana na utawala bora uliopo kwa sasa.

  Hayir alisema serikali inatumia fedha zake nyingi katika kuboresha ustawi wa vikosi vya usalama na kuwekeza katika elimu na afya.

  Alisema Somalia inafuata masharti yaliyowekwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa kanuni na usimamizi mzuri wa kifedha, na sasa wanatarajia msamaha wa mikopo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako