• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Tanzania kukarabati ndege zae ndani ya nchi

  (GMT+08:00) 2019-12-23 19:18:41

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Isack Kamwelwe, amesema kuanzia Januari Mwakani, ndege za Kampuni ya ATCL zitaanza kufanyiwa matengenezo ndani ya nchi kutokana na kukamilika kwa ukarabati wa 'hanga' lililopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA).

  Alisema pamoja na ukarabati huo, pia ununuzi wa mitambo mbalimbali unaendelea kufanyika kwa ajili ya kufanikisha matengenezo hayo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali kuhakikisha inaepukana na gharama za matengenezo ya ndege hizo nje ya nchi ambayo huigharimu fedha nyingi.

  Alisema katika kuhakikisha mpango huo unafanikiwa, hivi karibuni alitembelea hanga hilo na kujionea maendeleo na kujiridhisha kuwa limefikia katika hatua nzuri, tayari kwa kuanza kazi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako