• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenzake wa Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2019-12-23 19:38:49

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Korea Kusini Bw. Moon Jae-in katika Jumba la Mikutano la Umma mjini Beijing.

    Rais. Xi amesisitiza kuwa hivi sasa, vitendo vya kujilinda, upande moja na umwamba vinaendelea kusumbua usimamizi wa dunia na kutishia amani na utulivu wa dunia. Ikiwa ni nchi kubwa inayowajibika, China inadumisha kujiendeleza kwa kufuata mwenendo wa maendeleo ya dunia, kushirikiana na nchi mbalimbali kushikilia msimamo wa kunufaishana kwa usawa, kushauriana juu ya fursa na kutimiza majukumu kwa pamoja ili kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Pia amesema, China na Korea Kusini ni nchi muhimu za Asia na hata dunia, na katika miaka miwili iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo. Katika hali ya hivi sasa, pande hizo mbili zinapaswa kufikiria maslahi makuu na ufuatiliaji muhimu wa kila upande na kusukuma mbele uhusiano huo upande ngazi ya juu.

    Kwa upande wake, Bw. Moon amesema, Korea Kusini inatarajia pande hizo mbili zitaendelea kupanua ushirikiano wa sekta mbalimbali ikiwemo biashara, utamaduni, michezo, na uhifadhi wa mazingira. Bw. Moon pia amesema, masuala ya Hong Kong na Xinjiang yote ni mambo ya ndani ya China. Viongozi hao pia wamebadilishana maoni kuhusu hali ya peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako