• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Gor Mahia yaondoa hofu juu ya hatma ya kocha Polack

  (GMT+08:00) 2019-12-24 16:47:31

  Timu ya Gor Mahia ya Kenya imepinga fununu kuwa kocha wake Steven Polack, ambaye aliondoka nchini humo jumapili jioni kuelekea England kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas, hatarejea kwenye klabu hiyo katika muda wa wiki moja kama ilivyotarajiwa. Mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Lordvick Aduda amewataka mashabiki wa timu hiyo almaarufu K'ogalo kutulia, akisema kocha huyo atarejea Desemba 30 kwa kuwa bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo. Kabla ya kuondoka, Polack alishuhudia timu yake K'Ogalo ikiifunga Kisumu All Stars mabao 3 – 0 katika mechi ya Ligi Kuu Kenya iliyochezwa jumapili, hivyo kuirudisha timu hiyo kileleni mwa ligi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako