• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vijana watakiwa kutumia fursa ya michezo

  (GMT+08:00) 2019-12-24 16:48:17

  Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amewataka vijana kujikita katika kushiriki michezo na kutumia fursa wanazozipata ili kuimarisha vipaji vyao. Akizungumza na wanamichezo mbali mbali wa mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa mashindano ya 'VSSS Cup' ya ZSSF ya mfuko wa hifadhi ya jamii katika ukumbi wa Kariakoo Unguja. Alisema michezo imekuwa ikiwanyanyua vijana na kupata fursa za kimaisha pamoja na kujinusuru na vitendo vya uvunjifu wa amani,hivyo kuendelea kushiriki michezo na kuachana na mazingira yasiofaa katika jamii ni jambo muhimu. Hata hivyo alisema ni jambo la kuigwa na taasisi nyengine kwa 'VSSS' kuweza kufanya ubunifu kwa kuanzisha michezo kwani ni njia pekee ya kuwapatia fursa vijana kwa kusajiliwa katika timu kubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako