• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yakana tuhuma za kulazimisha wafungwa kuchapisha kadi za Krismas
     

    (GMT+08:00) 2019-12-24 19:07:09

    Mwenyekiti wa kampuni ya Uchapishaji ya Zhejiang Yunguang Bw. Lu Yunbiao amekana tuhuma za kulazimisha wafanyakazi kuchapisha kadi za Krismas ambazo husambazwa katika maduka makubwa ya manunuzi ya Tesco ya Uingereza, na kusema madai hayo ni ya uongo.

    Katika mahojiano maalum na CGTN, Bw. Lu amesema madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Uingereza kuwa kampuni hiyo imetumia wafungwa wa kigeni katika gereza la Shanghai Qingpu kama wafanyakazi hayana ukweli wowote. Amesema alishtushwa na taarifa hizo, kwa sababu kampuni yake haina utaratibu wa kufanya hivyo, na kuongeza kuwa hana namba ya simu ya gereza hilo wala anuani yake.

    Amesema kuwa bidhaa zote za Yungguang zinatengenezwa na wafanyakazi Wachina, wakifuata sheria na kanuni za ajira za China. Amesema, mchakato mzima wa utengenezaji wa kadi za Krismas ulifanywa na kampuni yake, kuanzia kuchapisha hadi kufungasha, na baadaye kuziweka kwenye makontena tayari kwa kusafirishwa nje.

    Kutokana na Bw. Lu, usafirishaji nje unachukua karibu asilimia 60 ya biashara ya kampuni hiyo, na wateja wa nje wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara na wa kushtukiza kila mwaka ili kukagua masuala ya haki za binadamu, ulinzi wa mazingira, na vifaa vya kuzimia moto. Amesema wateja wote wa nje wa kampuni hiyo wanawafanyia uchunguzi japo mara moja kwa mwaka, na ni uchunguzi wa ghafla. Kutokana na mikataba waliyofikia, kampuni ya Bw. Lu inapaswa kuwa wazi kwa wateja katika nyanja zote, na pia wanaweza kukagua computer zao.

    Jumapili iliyopita, aliyekuwa mwandishi wa habari aitwaye Peter Humphrey, ambaye alifungwa gerezani China kwa miezi 23, miezi tisa katika gereza la Qingpu, alidai kuwa mtoto mdogo wa kike wa miaka sita alipokea ujumbe uliofichwa kwenye kadi ya Krismas iliyotengenezwa na wafungwa katika gereza Shanghai Qingpu. Alisema ujumbe huo ulitoka kwa wafungwa waliokuwa wanamfahamu kabla ya hajaachiwa huru, waliodai kuwa walikuwa wanalazimishwa kufanya kazi kinyume na matakwa yao.

    Siku hiyohiyo, Tesco ilitoa taarifa kuwa kampunia ya Uchapishaji ya Zhejiang Yungpung inafanyiwa ukaguzi huru, na mara ya mwisho ilikaguliwa mwezi uliopita, na kulikuwa hakuna ushahidi kuwa wamevunja sheria inayokataza matumizi ya wafungwa. Taarifa hiyo pia ilisema Tesco ilishtushwa na ripoti hiyo na kuahirisha uzalishaji wa kadi za Krismas uliokuwa unafanywa na kampuni hiyo.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Suang amepuuza tuhuma hizo, akiziita kuwa ni za uongo zilizofanywa na Humphrey. Ameongeza kuwa anatumaini Humprey ataacha kutafuta umaarufu kwa kusema habari zinazoichafua China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako