• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China, Japan na Korea ya Kusini zahimizwa kushirikiana kuzidisha ustawi na utulivu wa kikanda

    (GMT+08:00) 2019-12-24 19:08:16
    Mkutano wa nane wa viongozi wa China, Japan na Korea ya Kusini umefanyika leo mjini Chengdu, China, na kuhudhuriwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang, rais Moon Jae-in wa Korea ya Kusini na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe. Kwenye mkutano huo Bw. Li amehimiza nchi hizo kushirikiana ili kuzidisha ustawi na utulivu wa kanda ya Asia ya mashariki.

    Mkutano huo umefanyika wakati ikitimia miaka 30 tangu China, Japan na Korea ya Kusini zianzishe ushirikiano wa pande tatu. Bw. Li anasema,

    "Tuna maoni ya pamoja kwamba, nchi zetu zinapaswa kuaminiana zaidi katika mambo ya kisiasa, na kushikilia mwelekeo wa ushirikiano. Sote tunapenda kufikiria ushirikiano kati ya China, Japan na Korea ya Kusini kwa mtizamo wa kimkakati na wa muda mrefu, kuzingatia historia, kuanzisha mustakabali, na kuongeza maslahi ya pamoja."

    Ili kukuza ushirikiano, Bw. Li amependekeza nchi hizo kuimarisha msingi wa kuaminiana, kuheshimu maslahi makuu na mambo muhimu yanayofuatiliwa na nchi nyingine. Anasema,

    "Sote tunatetea kusaini makubaliano ya kikanda ya wenzi wa ushirikiano wa kiuchumi katika pande zote (RCEP) mapema iwezakanavyo, na pia tumeahidi na kupenda kusukuma mbele ujenzi wa eneo la biashara huria kati ya China, Japan, na Koreaya Kusini. Ujenzi wa maeneo ya biashara huria si kama tu utalinda biashara huria na kunufaisha amani ya dunia, bali pia utasaidia kuhimiza mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani."

    Bw. Li amesisitiza kuwa, hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa, China, Japan na Korea ya Kusini zinapaswa kuongeza ushirikiano ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja, na kutoa mchango kwa ajili ya ustawi na utulivu wa kikanda na kimataifa.

    Kwa upande wake, rais Moon amesema nchi hizo zinapaswa kushirikiana kwa karibu, kuongeza maslahi ya pamoja kwa hatua mfululizo, na kufanya ushirikiano katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi, mazingira, afya, uzeeni na mengineyo. Amesisitiza kuwa Korea ya Kusini inapenda kushirikiana na pande nyingine kutimiza hali ya kutokuwepo kwa silaha za nyukilia katika peninsula ya Korea, na kudumisha amani na utulivu wa peninsula hiyo.

    Naye Bw. Abe amesema, Japan, China na Korea ya Kusini zinapaswa kujumuisha uzeofu, na kutunga mpango wa ushirikiano katika mwongo ujao, ili kuleta mafanikio ya pande tatu. Ameongeza kuwa nchi hizo zina historia ndefu ya mawasiliano ya ustaarabu, na zinapaswa kusukuma mbele ushirikiano katika mambo ya michezo, utalii na utamaduni. Amesisitiza kuwa Japan itajitahidi kushirikiana na China na Korea ya Kusini kulinda biashara huria, utaratibu wa pande nyingi, na kulinda mazingira ya kibiashara yenye haki na usawa bila ya ubaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako