• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Manchester United ipo kwenye hatihati ya kumpoteza nyota wao kinda Angel Gomez

  (GMT+08:00) 2019-12-25 09:16:04

  Manchester United ipo kwenye hatari ya kumpoteza nyota wao kinda Angel Gomez mwenye mpango wa kwenda ndani ya kikosi cha Barcelona. Kinda huyo mwenye miaka 19 amesema kuwa ana mpango wa kuondoka ndani ya Old Trafford ili kutimiza malengo yake aliyojiwekea baada ya kushindwa kufikia makubaliano na mabosi wa United. Gomez anayekipiga pia kwenye timu ya taifa ya England ya chini ya miaka 20 alianza kulelewa ndani ya United akiwa na miaka sita amecheza jumla ya mechi saba za wakubwa na alianza tatu pekee za kwenye Ligi ya Europa. Habari zinaeleza kuwa mbali na Barcelona ambako anacheza mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi pia Juventus na Craystal Palace zimeonyesha nia ya kuipata saini ya kinda huyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako