• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Sven Vandenbroeck wa Simba asema anataka mshambuliaji asilia

  (GMT+08:00) 2019-12-25 09:16:36

  Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck, amesema anataka mshambuliaji asilia katika dirisha dogo la usajili. Sven ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuiongoza Simba kupata ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya AFC Arusha katika mchezo wa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, juzi. Hii ni mara ya kwanza kocha huyo kuzungumzia usajili tangu alipotwaa mikoba ya Patrick Aussems ambaye mkataba wake ulisitishwa. Tayari Simba imeanza mchakato wa kumsajili winga wa UD Songo, Luis Jose ambaye pia ana uwezo wa kucheza nafasi ya mshambuliaji. Sven alisema ameona wachezaji 19 tangu alipoanza kazi na amebaini ubora na kasoro zao. Aidha amevutiwa na kiwango cha Meddie Kagere, lakini John Bocco na Wilker Da Silva hawako imara kwa ushindani, hivyo anahitaji kuongeza nguvu katika eneo hilo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema sven amepewa jukumu la kusajili aina ya mchezaji anayemtaka na uongozi utamuunga mkono.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako