• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kibarua cha Kocha Javier Martinez wa Rayon Sports ya Rwanda chaota mbawa

  (GMT+08:00) 2019-12-25 09:17:03

  Kocha Javier Martinez Espinosa amefutwa kazi kama kocha mkuu wa Rayon Sports ya Rwanda kufuatia kichapo cha 2-0 dhidi ya mahasimu wao wakubwa APR kwenye Ligi Kuu ya Rwanda wikiendi iliyopita. Mmexico huyo aliyejiunga na klabu kwa mkataba wa mwaka mmoja kabla ya kuanza kwa msimu wa 2019-20, anaondoka kwenye klabu baada ya kukinoa kikosi kwa miezi mitatu tu. Rayon wamethibitisha hayo kupitia akaunti yao rasmi ya Twitter ya klabu hiyo jana Jumanne. Martinez alisainiwa September, ambapo alichukua nafasi ya Mbrazili Roberto Oliveira aliyeiongoza klabu na kuitwaisha taji lake la tisa mwezi Juni. Kwa mujibu wa Jean Paul Nkurunziza, msemaji wa Rayon Sports, kocha msaidi wa zamani Alain Kirasa ndio amechukua mikoba kwa muda hadi atakapopatikana kocha mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako