• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KIKAPU: Kikosi cha Morans cha Kenya chaongezewa nguvu ya wachezaji watatu

  (GMT+08:00) 2019-12-25 09:17:33

  Wachezaji wengine watatu wanahushishwa kuongezwa kwenye timu ya wanaume ya kikapu ya Kenya Morans wakati kikosi kitakaporejea tena kambini kujiandaa na michuano ya kabla ya kufuzu mashindano ya mabingwa wa Afrobasketball 2020 yatakayofanyika mwezi ujao mjini Nairobi. Timu inavunja kambi kwa siku tatu kuanzia leo Jumatano na itarejea tena Ijumaa. Kocha mkuu Cliff Owuor amesema amewajumuisha James Mwangi wa Ulinzi Warriors, Ariall Ortega na Mike Makiada. Timu imekuwa kwenye mazoezi kwa wiki mbili zilizopita. Amesisitiza kuwa amewaita wachezaji hao kwa manufaa ya timu na sio kutokana na shinikizo kutoka upande wowote. Mashindano hayo yataishuhudia Kenya ikipambana na Tanzania, Burundi, Eritrea na Sudan Kusini ili kujikatia tiketi moja ya kushiriki ya michuano ya kufuzu Afrobasketball mwezi Machi. Uganda na Rwanda, za Zoni ya mataifa mengine matano, zimejikatia tiketi moja kwa moja kwa vile zilishiriki kwenye makala iliyopita ya mabingwa wa Afrobasket.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako