• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Habari za kupotosha ukweli huwa na madhumuni maovu

    (GMT+08:00) 2019-12-25 09:38:34

    Hivi karibuni aliyekuwa mwanahabari wa Uingereza aliyewahi kutumikia kifungo hapa nchini China Peter Humphrey alitoa makala kwenye gazeti la Sunday Times, akisema msichana wa London mwenye miaka sita kwenye kadi ya Krismasi aliyonunua kutoka kwenye supamaketi ya Tesco, aligundua maandishi ya kiingereza yanayosema "Sisi ni wafungwa wa kigeni kwenye gereza la Qingpu mjini Shanghai, tumelazimika kufanya kazi za sulubu. Tafadhali tusaidie na kuripoti kwa mashirika ya haki za binadamu." Baadaye, habari hiyo ya ajabu iliripotiwa na vyombo vingi vya habari vya Magharibi ikiwemo BBC na Sky News, vikishambulia na kuipaka matope China.

    Ukweli ni kwamba kampuni ya China iliyotengeneza kadi hizo za Krismasi zinazouzwa kwenye supamaketi ya Tesco imeweka bayana kuwa kamwe haikuwahi kuwa na ushirikiano wowote na gereza la Qingpu, na kadi hizo zilizotolewa kwa Tesco zote zilitengenezwa na wafanyakazi wachina ndani ya kiwanda cha kampuni hiyo. Wakati huohuo Supamaketi ya Tesco pia imetoa taarifa kwa wanahabari ikisema kuwa "hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa watengenezaji wa bidhaa zinazouzwa kwenye Tesco wamekiuka marufuku ya kutumikisha wafungwa wa gerezani." Wizara ya mambo ya nje ya China pia imejibu kuwa gereza la Qingpu kamwe halijawahi kuwalazimisha wafungwa wa kigeni kufanya kazi.

    Ukweli umethibitha kuwa tuhuma zilizotolewa na Peter Humphrey hazina msingi wowote wala hazina ushahidi wowote.

    Kwa kweli watu wenye mantiki hata kidogo hawawezi kuamini habari feki zilizotolewa na Peter Humphrey, kutokana na historia yake chafu ya kuhusika na uhalifu mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwenye tovuti ya Wizara ya Usalama wa Umma ya China, tangu mwaka 2003 Peter Humphrey na mkewe walikusanya kiharamu na kuuza taarifa binafsi za raia wa China, kwa ajili ya kupata faida za kiuchumi. Mwaka 2013, Humphrey alikamatwa na polisi wa China, akahukumiwa kifungo cha miezi tisa kwenye gereza la Qingpu kabla ya kuachiwa huru mwaka 2015. Baada ya hapo, akajitokeza mara kwa mara kuishambulia na kuipaka matope China, ili kujipatia faida za kiuchumi.

    Lakini kwanini habari kama hiyo ambayo inatambuliwa kirahisi kuwa ni ya feki, inatangazwa sana na vyombo vya habari vya magharibi? Hali hii inadhihirisha kuwa, uhasama wa baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi dhidi ya China uko kwenye damu yao, na hata wanaweza kuachana na maadili ya kimsingi ya kitaaluma na kupuuza ukweli, ili kutumia njia yoyote kadri wanavyoweza kuishambulia China.

    Mtu yeyote kweli akitaka kuifahamu China ilivyo, anaweza kuja na kujionea mwenyewe, uvumi na habari feki kamwe haviwezi kubadilisha ukweli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako