• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China, Korea Kusini na Japan zakubaliana kuimarisha ushirikiano katika muongo ujao

    (GMT+08:00) 2019-12-25 09:44:48

    China, Korea Kusini na Japan zimeeleza matarajio ya ushirikiano kati ya pande tatu katika muongo ujao na Miradi ya ushirikiano kati ya pande hizo tatu na pande nyingine, na kuahidi kuimarisha ushirikiano kati yao kwenye sekta mbalimbali.

    Makubaliano hayo yamefikiwa na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, rais Moon Jae-in wa Korea Kusini na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe walipohuduria mkutano wa 8 wa viongozi wa China, Japan na Korea Kusini uliofanyika huko Chengdu, China.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema, China, Japan na Korea Kusini ni wenzi muhimu wa maendeleo, wanaosaidiana kiuchumi na sekta zao zinaungana. Amesema licha ya kukabiliana na changamoto, pande hizo tatu zinafanya juhudi kupata maendeleo ya pamoja na kutatua migongano kwa njia ya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako