• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza umuhimu wa misaada ya kijamii katika vita dhidi ya umaskini

    (GMT+08:00) 2019-12-25 16:39:26
    Baraza la Serikali la China leo limekabidhi ripoti kwa mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, ili kujulisha maendeleo ya utoaji wa misaada ya kijamii, na vita dhidi ya umaskini.

    Katika vita dhidi ya umaskini, kuna watu wasio na uwezo wa kufanya kazi, hata kuishi kwa kujitegemea, na watu hao hawawezi kuondokana na umaskini kupitia sera ya kuendeleza sekta za kiuchumi. Hivyo kuwapatia misaada ya kijamii ni muhimu kwa juhudi za kushinda vita dhidi ya umaskini. Waziri wa mambo ya umma wa China Bw. Li Jiheng anasema,

    "Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, China imeharakisha kuendeleza misaada ya kijamii, na kutenga fedha nyingi zaidi hatua kwa hatua, ili kuinua kiwango cha misaada hiyo. Misaada hiyo imetoa uhakikisho wa kimsingi kwa maisha ya mamilioni ya watu maskini mijini na vijijini nchini China."

    Misaada ya kijamii ni mfumo unaotekelezwa na serikali ya China kwa ili kutimiza mahitaji ya kimsing ya maisha ya watu maskini. Kwa mujibu wa "kanuni ya muda ya misaada ya kijamii" iliyotungwa mwaka 2014 na Baraza la Serikali la China, misaada hiyo inahusisha chakula, mavazi, matibabu, elimu, nyumba, na ajira kwa watu maskini zaidi, na misaada ya muda kwa watu walioathirika na maafa. Kuhusu hatua zijazo za kuendeleza misaada ya kijamii, ripoti hiyo inasema China itafanya vizuri kazi za kuhakikisha maisha ya kimsingi ya watu maskini, ili kushinda vita dhidi ya umaskini. Bw. Li anasema,

    "Tutafanya vizuri kazi mbalimbali katika kipindi cha mwisho cha vita dhidi ya umaskini, ili kuhakikisha malengo yanatimizwa kiuhalisi. Tutaimarisha uwezo wa kuhakikisha maisha ya kimsingi ya watu maskini vijijini, na kujenga na kukamilisha utaratibu wa muda mrefu wa kutokomeza umaskini, ili kukinga watu walioondokana na umaskini kurudi kuwa maskini."

    Aidha, China pia itatoa misaada maalumu ya matibabu, nyumba, elimu na ajira kwa familia yenye kipato chini na malipo makubwa ya lazima.

    Kuhusu vitendo vya kutapeli ruzuku za serikali, ripoti hiyo inasema katika miezi 9 ya mwanzao ya mwaka huu, idara za mambo ya umma katika ngazi mbalimbali ziligundua kesi 1,319, ambazo zinawahusisha maofisa 705. Bw. Li anasema,

    "Tutashikilia mstari wa mwisho, kuendelea kuimarisha usimamizi wa bajeti ya misaada ya kijamii, na kuadhibu vitendo vinavyo kiuka sheria. Licha ya hayo, tutafungua njia za kuripoti vitendo hivyo, kuanzisha ushirikiano kati ya idara za misaada ya kijamii na idara za sheria, na kuimarisha ujenzi wa mfumo wa uaminifu wa misaada ya kijamii."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako