• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • BASKETBALL: Mtaka Taifa Cup kufanyika Simiyu December 27 hadi 31

  (GMT+08:00) 2019-12-25 17:57:57

  Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) linatarajia kuwa na Mashindano ya kombe la Taifa la Kikapu (Mtaka Taifa Cup 2019) yatafanyika mkoani Simiyu tarehe 27 hadi 31 Dec 2019 sambamba na mkutano mkuu wa mwaka. Kwa mujibu wa Rais wa TBF, Phares Magesa amesema kuwa Mashindano haya yatashirikisha timu za mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani za wanawake na wanaume. Aidha, mbali na michuano hiyo, TBF inatarajiwa kufanya Mkutano wake Mkuu Desemba 29, pamoja na mambo mengine huku pia kukitarajiwa kuwa na semina kwa viongozi wote wa vyama vya mikoa na Taifa kuhusu Uongozi, utawala na masoko. Rais huyo wa TBF aliipongeza timu ya Kikapu ya JKT ambayo imetuwakilisha katika mashindano ya kufuzu kucheza ligi ya Kikapu Afrika 'Basketball Africa League (BAL)' yaliyofanyika Kigali Arena, Rwanda 17-22 mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako