• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kocha Mbeya City ataja mbinu iliyoibana Yanga

  (GMT+08:00) 2019-12-25 18:03:32

  Wakati kocha wa Yanga Charles Boniface Mkwassa akitaja sababu mbili zilizochangia timu yake kupata suluhu, kocha wa Mbeya City Amri Said amesema mbinu ya kupaki basi ilimsaidia kupata matokeo hayo. Amri amesema, anatambua kuwa Yanga ni timu bora, hivyo aliwaandaa wachezaji wake kucheza kwa kujilinda ili kuwabana wapinzani wao wasipate bao. Amesema mbinu hiyo ilichangia Yanga kucheza kwa presha, hatua iliyowalazimisha kutumia nafasi hiyo kufanya mashambulizi ya kushtukiza. Kwa upande wake, Mkwasa amesema licha ya wachezaji wake kupambana ili kupata ushindi, lakini uwanja na uamuzi vilikuwa vikwazo kwao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako