• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bei ya nyama ya mbuzi na kuku yapanda

  (GMT+08:00) 2019-12-25 18:07:30

  Bei ya mbuzi na kuku imepanda zaidi wakati huu wa Krismasi huku uchumi ukishuhudia kupungua kwa watu wanaonunua kuwageuza kitoweo.

  Mbuzi mzima katika soko maarufu ya nyama ya mbuzi ya Kiamaiko, katika mtaa wa Huruma, Nairobi inauzwa kwa Sh8,000 kutoka bei ya kawaida ya Sh4,000 huku wafanyabiashara wakiimarisha mauzo yao wakati huu wa msimu wa sherehe.

  Bei ya kuku katika soko la Burma, Nairobi imepanda na kufikia kati ya Sh1,300 na Sh1,500 kutoka bei ya kawaida ya wastani ya Sh1,000.

  Kupanda huku kwa bei kunajiri wakati ambapo uchumi nchini umezorota. Wafanya biashara wengi wanasema biashara katika msimu wa mwaka huu sio nzuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Nyama ya mbuzi na kuku hupendwa zaidi na Wakenya wakati kama huu wa msimu wa sherehe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako