• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima 10,000 kunufaika na Mradi wa kilimo trust

  (GMT+08:00) 2019-12-25 18:07:51

  Zaidi ya wakulima 10,000 wa mpunga wa vijiji 26 katika wilaya ya Rungwe, wanatarajiwa kunufaika na Mradi wa Kilimo Trust unaoendeshwa na kiwanda cha kusindika mpunga cha Kyela Rice.

  Kiwanda hicho kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo kinaandaa mashamba darasa kwa ajili ya kuwaelimisha wakulima namna bora ya kuzalisha zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kuimarisha soko la zao hilo ndani na nje ya nchi.

  Msimamizi wa Kilimo Trust, Thobias Mwankonda, amesema mradi huo unalenga kutoa elimu ya kilimo bora cha mpunga kupitia mashamba darasa 50 ambayo yataanzishwa kwenye vijiji.

  Alisema wanataka kuwaondoa wakulima kwenye kilimo cha mazoea ambacho tija yake ni ndogo hasa katika kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya tano inasisitiza kuingia kwenye uchumi wa kati unaoambatana na mapinduzi ya viwanda.

  Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Moses Mwaipopo, alisema wamefikia hatua hiyo ya kumwinua mkulima mdogo kutokana na uhitaji mkubwa wa soko la mchele unaotoka Kyela ndani na nje ya nchi.

  Alisema kila sehemu kwenye masoko ya mpunga inaonyesha mchele kutoka Kyela ndio wenye soko zuri kuliko unaozalishwa katika maeneo mengine, lakini kiwango cha uzalishaji bado hakikidhi mahitaji hayo ya soko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako