• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanya biashara wa huduma za usafiri wafurahia biashara

  (GMT+08:00) 2019-12-25 18:08:12

  Wafanya biashara za uchukuzi nchini Uganda walionekana kufurahia faida kubwa wakati huu ambapo watu wen gi nchini humo wanasafiri vijijini kwa sherehe za krismasi na mwaka mpya. Wamiliki wa mabasi ya usafiri wanasema biashara imekuwa nzuri kwa kuwa wafanya biashara wa vijijini pia wanasafirisha bidhaa nyingi kutokana na mahitaji ya watu vijijini. Wamiliki wa magari ya texi pia walionekana kufurahia biashara katika mji wa Kampala kwa kuwa baadhi ya watu waliamua kutumia magari hayo baada ya mabasi kujaa. Hata hivyo wamiliki wa magari ya Texi wanasema wengi wao wana wasiwasi hasa wanaposafiri mbali kutokana na suala la usalama na pia miundo mbinu ambayo bado sio mizuri hasa barabara zisizopitika. Wakati huo huo nchini Rwanda watu wengi walionekana wakisafiri kwenda vijijini kujumuika na jamaa zao kwa sherehe za krismasi na mwaka mpya. Wafanya biashara wa kutoa huduma za usafiri walionekana wakifurahia biashara huku maofisa wa usalama wakiendelea kuimarisha usalama barabarani. Viongozi wa nchi za Afrika mashariki wamewataka madereva wa magari ya usafiri kuwa makini barabarani wakati wanapowasafirisha watu vijijini kwa sherehe za krismasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako