• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawaziri wakuu wa China na Japan wafanya mazungumzo

  (GMT+08:00) 2019-12-25 18:45:32

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amekutana na mwenzake wa Japan Bw. Shinzo Abe leo mjini Dujiangyan, kusini magharibi mwa China.

  Bw. Li ametoa wito kwa China na Japan kufuata kanuni zilizoamuliwa kwenye nyaraka nne za kisiasa kati ya nchi hizo, kuendelea na moyo wa kujifunza kutokana na historia na kuangalia siku zijazo, kutatua masuala nyeti kwa njia mwafaka na kuhimiza uhusiano wao kupata maendeleo mapya. Amesema China na Japan ni wenzi muhimu wa kibiashara, na China inafungua zaidi soko la sekta ya huduma kwa nje, jambo ambalo litatoa fursa kubwa kwa nchi hizo katika kushirikiana.

  Bw. Li ameongeza kuwa mkutano wa nane wa wakuu wa China, Japan na Korea Kusini umetoa ishara chanya za kulinda utaratibu wa pande nyingi na bishara huria na kulinda amani na utulivu wa kikanda. China inapenda kuongeza mawasiliano na uratibu na pande mbalimbali ikiwemo Japan, ili kuhimiza "Makubaliano ya Uhusiano wa Wenzi wa Kiuchumi wa Pande Zote wa Kikanda" RCEP kusainiwa mwakani na kuongeza kasi ya mazungumzo kuhusu makubaliano ya eneo la biashara huria kati ya China, Japan na Korea Kusini.

  Bw. Shinzo Abe amesema Japan inapenda kushiriki katika mchakato wa China wa kufungua soko lake la sekta ya huduma. Pia Japan inapenda kufanya juhudi na China kuhimiza kusainiwa kwa RCEP na mchakato wa mazungumzo kuhusu eneo la biashara huria kati ya Japan, China, na Korea Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako