• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yafikiria kuondoa askari wake kutoka nchi za Afrika magharibi

  (GMT+08:00) 2019-12-25 19:22:34

  Gazeti la New York Tims jana liliripoti kuwa, waziri wa ulinzi wa taifa wa Marekani Bw. Mark Esper anafikiria mpango wa kuondoa askari wa nchi hiyo kutoka nchi za Afrika magharibi, ambao ni sehemu moja ya mpango wa kupunguza tena askari 200,000 waliopo nchi za nje.

  Likiwanukuu maofisa wenye ufahamu wa ndani kuhusu suala hilo, Gazeti hilo limesema Bw. Esper anafikiria kukitelekeza kituo cha ndege zisizo na rubani kilichojengwa hivi karibuni nchini Niger kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 110, na kumaliza msaada wake kwa jeshi la Ufaransa linalopambana na makundi yenye silaha katika nchi za Mali, Niger na Burkina Faso.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako