• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa viongozi kati ya China, Japan na Korea Kusini waimarisha hali ya kuaminiana na ushirikiano

  (GMT+08:00) 2019-12-26 08:52:15

  Mkutano mpya kati ya viongozi wa China, Japan na Korea Kusini umetajwa kuwa umeimarisha hali ya kuaminiana na ushirikiano kati ya pande hizo tatu.

  China, Japan na Korea Kusini Jumanne wiki hii zilitoa Ruwaza ya Ushirikiano wa Pande Tatu katika Muongo Ujao na Miradi ya ushirikiano kati ya pande hizo tatu na nyingine (Trilateral + X) kwenye mkutano wa awamu ya nane kati ya viongozi wa nchi hizo tatu uliofanyika mjini Chengdu, kusini magharibi mwa China.

  Profesa Liu Di wa taasisi ya Sayansi Jamii katika Chuo kikuu cha Kyorin mjini Tokyo amesema mkutano huo umetambulisha mara nyingine tena ushawishi wa nchi hizo tatu katika masuala ya kikanda na ya kimataifa, na kwamba katika miaka 20 iliyopita, mafanikio makubwa yamepatikana kwenye ushirikiano kati ya pande hizo tatu, ambao umechukua nafasi muhimu katika kuelekeza maendeleo ya uchumi wa dunia kwenye njia sahihi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako