• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Victoria Conteh ateuliwa kuwa kocha wa kwanza mwanamke wa klabu ya East End Tigers

  (GMT+08:00) 2019-12-26 09:16:00
  Victoria Conteh ameteuliwa kuwa kocha wa kwanza mwanamke kuifunza klabu ya wanaume katika ligi ya Sierra Leone kwa sababu amefuzu kufanya hivyo. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 ni mwanamke wa pili kusimamia klabu ya ligi ya daraja la juu ya wanaume barani Afrika baada ya mwanamke mwengine wa Ethiopia kocha Meseret Manni aliyeifunza klabu ya wanaume ya Dire Dawa mwaka 2015. Klabu ya East End Tigers wamemuajiri mchezaji huyo wa zamani kwa kipindi cha miaka miwili. Mmiliki wa klabu hiyo Victor Lewis amesema sio kuchagua mwanamume ama mwanamke kigezo chao ni kufuzu kufanya kazi hiyo na kwamba wamempa mkataba wa miaka miwili na kumuwekea lengo lao la kumaliza katika timu nne bora. Conteh ndio kocha mwanamke wa pekee aliyepewa leseni na Caf katika taifa hilo na awali alikuwa akiifunza timu ya taifa ya wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 mbali na timu ya wanawake ya polisi wa Sierra leone. Lakini sio mgeni kwa mchezo wa wanaume, baada ya kuisimamia kwa muda klabu ya wanaume iliyopo katika ligi ya pili Delta Strikers. Katika mechi yake ya kwanza Conteh alipata sare ya 1-1 akiifunza East End Tigers.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako