• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Jurgen Klopp awapa tano wachezaji wake kwa kupambana kiume fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Duniani

  (GMT+08:00) 2019-12-26 09:16:27

  Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema wachezaji wake walipambana mbele ya timu bora kwenye fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Duniani dhidi ya Flamengo. Liverpool Jumamosi usiku iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Flamengo na kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa kombe la klabu bingwa duniani. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Roberto Firmino kwenye muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare tasa. Klopp amesema ni maajabu kuona namna gani wachezaji wake wameshinda, walicheza na wachezaji ambao wana uwezo mkubwa jambo ambalo liliwafanya wapate taabu kupata matokeo mapema. Kwa sasa amesema wana ratiba ngumu kwani wana mchezo dhidi ya Leicester City ambao ni wa ligi ila amesisistiza kuwa hawana namna isipokuwa kupambana tu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako