• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Saul Alvarez atajwa bondia namba moja duniani katika kila uzani akimpiku Anthony Joshua

  (GMT+08:00) 2019-12-26 09:16:57

  Wakati Hassan Mwakinyo akitakata kwa mabondia wa Bongo, bingwa wa dunia, Anthony Joshua (AJ) amefunikwa na Saul Alvarez katika ubora wa dunia kwenye orodha ya mabondia bora wa dunia wa uzani tofauti (Lb for Lb). Katika rekodi hiyo iliyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (boxrec) unaohusisha mabondia wa uzani wa hadi ule wa chini Alvarez ambaye ni bondia namba moja kwenye uzani wa juu mwepesi (light heavy) ametajwa kuwa bondia namba moja wa dunia katika kila uzani akiwapiku wengine 18,202 wanaotambulika duniani. Alvarez amewafunika nguli wa ngumi duniani akiwamo bondia namba moja wa uzani wa juu, Anthony Joshua ambaye katika viwango vya Lb for Lb ametajwa kuwa bondia namba nane akifuatiwa na Manny Pacquiao ambaye ni kinara kwenye uzani wa welter lakini amekamata nafasi ya tisa Lb for Lb. Terence Crawford (uzani wa welter) amekamata nafasi ya pili, akifuatiwa na Gennadiy Golovkin (middle), Errol Spence Jr (welter), Vasiliy Lomachenko (light), Miguel Berchelt (super feather) Callum Smith (super middle), Joshua (heavy), Pacquiao (welter) na Shawn Porter anayepigana kwa uzani wa welter akihitimisha 10 bora. Kwa mabondia wa Tanzania, katika viwango hivyo, Hassan Mwakinyo anayepigana kwa uzani wa super welter ndiye ameng'ara akiwa bondia wa 261 duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako