• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Kikosi cha ndondi Taifa chaTanzania kuanza kampeni ya kushiriki michezo ya Olimpiki 2020

  (GMT+08:00) 2019-12-26 09:17:26

  Baada ya kukosa nafasi ya kushiriki michezo ya Olimpiki ya msimu uliopita, kikosi cha ndondi Taifa nchini Tanzania kimerejea upya kwenye mchakato huo. Mabondia wa timu ya Taifa leo Alhamisi watakuwa na kibarua cha kutetea nafasi zao watakapoanza kupanda ulingoni kuzichapa katika mashindano ya kimataifa ya Bingwa wa Mabingwa mkoani Arusha. Mabondia hao watachuana na wenzao ambao hawakuitwa kwenye timu ya Taifa sanjari na wengine kutoka nchi za Kenya na Uganda ikiwa ni moja ya mechi ambazo kocha mkuu wa timu ya Taifa David Yombayomba ameomba ili kupima viwango vya mabondia wake. Baada ya mashindano hayo yatakayofikia tamati Desemba 31, timu hiyo itachuana kwenye mashindano mengine ya kimataifa nchini yatakayohusisha mabondia wa Afrika mashariki wanaojiandaa kwenda Dakar Senegal kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kufuzu Olimpiki 2020. Mashindano ya Senegal ndiyo pekee yanayotoa viwango vya olimpiki kwa mabondia wa Afrika, mashindano hayo yatasimamiwa na kamati maalumu iliyoundwa na kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) baada ya mgogoro baina yake na Shirikisho la ngumi za ridhaa la kimataifa (AIBA).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako