• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba SC yaendeleza kichapo ligi kuu ya Tanzania bara kwa kuitandika lipuli fc 4-0 uhuru

  (GMT+08:00) 2019-12-26 09:18:04

  Mabingwa watetezi, Simba SC wameendeleza 'dozi' baada ya jana kuwachapa Lipuli FC ya Iringa 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Ushindi huo wa pili mfululizo chini ya kocha mpya, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck unaifanya Simba SC ifikishe pointi 28 katika mchezo wa 11 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya Kagera Sugar inayofuatia ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.

  Ikitoka kuichapa AFC ya Arusha 6-0 katika mchezo wa kwanza chini ya Vandenbroeck, Simba SC jana iliendelea kucheza soka safi ya pasi za haraka na kasi ya kushambulia kiasi cha kuwazidi kabisa wapinzani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako