Kocha wa Chelsea Frank Lampard amempiga kijembe Jose Mourinho akiponda uamuzi wake wa kuwaruhusu wachezaji nyota Kevin De Bruyne na Mohamed Salah waondoke Stamford Bridge. Mourinho ambaye kwa sasa ni kocha wa Tottenham Hotspur alifanya kazi na nyota hao wawili katika kipindi chake cha pili alichokuwa kwenye kikosi cha Chelsea, lakini wachezaji wote hao walionekana kuwa hawajui na hivyo kuondolewa kwenye timu. Mwaka 2014 De Bruyne alikwenda Wolfsburg kwa ada ya pauni milioni 18 na Salah AS Roma mwaka 2016 kwa ada ya pauni milioni 12. Lakini baadaye wachezaji hao walirejea EPL, Bruyne akitua Man City na Salah akisaini na Liverpool, na kwa sasa ni wachezaji mahiri kwenye timu husika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |